PEMBEJEO ZA RUZUKU MSIMU WA KILIMO 2015/2016 ILIKUWA CHANGAMOTO TUPU KWA WAKULIMA MANISPAA YA MPANDA
WAKATI msimu wa kilimo wa mwaka
2016/2017 ukitarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu,ripoti ya matumizi ya
pembejeo Katika msimu uliopita wa 2015/2016 katika Manispaa ya Mpanda imeonesha
kuwa ilitumia jumla ya pembejeo 27813 kati ya 32145 zilizoletwa katika Manispaa
hiyo zimetumika.
Tarifa ya Kaimu Afisa kilimo Manispaa
ya Mpanda Bw. Said Hemed iliyotolewa na Afisa habari wa Manispaa ya Mpanda
Bw.Donald Pius ilionesha kuwa matumizi ya pembejeo katika msimu wa kilimo
uliopita hayakutumika ipasavyo na kwa wakati kwa madai kuwa wizara ya kilimo kuchelewesha
pembejeo hizo.
Baadhi ya wakulima Katika Manispaa ya
Mpanda Bernard Nkana na Kapata Joseph walisema kuwa wamekuwa wakipata hasara
kubwa ya sekta ya kilimo kutokana na pembejeo za kilimo kucheleweshwa.
Aidha walisema mbali na kucheleweshwa
kwa mbolea na mbegu bado bei ya pembejeo hizo ni kubwa
ukilinganisha na uwezo wa mkulima ambapo wametolea mfano kuwa bei ya mbolea CAN na UREA ni shilingi 58,000/=.
Hata hivyo mawakala wasambazaji wa
pembejeo za ruzuku wanalalamikiwa na wakulima kwa kutosambaza pembejeo hizo kwa
wakati suala ambalo miongoni mwa mawakala waliozungumza na mtandao huu walisema
kuwa tatizo la kuchelewa kwa pembejeo za kilimo siyo lao bali ni la serikali
kuchelewa kuwakabidhi mbolea hizo.
Akitolea ufafanuzi wa mbegu na mbolea
kuwa na bei ya juu,Afisa habari wa Manispaa Bw.Donald Pius kwa niaba ya Kaimu afisa
kilimo Manispaa ya Mpanda alisema kuwa ndiyo bei elekezi ya serikali ambapo
hata hivyo walisema kuwa wataishauri serikali kuleta mbolea mapema sanjari na
kupitia upya gharama za pembejeo za kilimo.
Katika takwimu ya vocha za ruzuku
zilizopokelewa na Manispaa zinaonesha kuwa mbolea ya kupandia zilikuwa
10,644,Mbolea ya kukuzia zilikuwa 10,644,mbegu za mahindi chotara 10,644 na
mbegu za Mpunga 213 huku mbolea zilizotumika zinaonesha kuwa mbolea ya kupandia
zilikuwa 9200, Mbolea ya kukuzia zilikuwa 9200, mbegu za mahindi chotara 9200
na mbegu za Mpunga 213
Miongoni mwa mazao yanayolimwa Mkoani
Katavi kwa wingi ni pamoja na Mahindi,mihogo,mpunga,ulezi,ufuta na karanga.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments