WIZI WA SHUKA,GODORO NA FEDHA VYAMFIKISHA MAHAKAMANI MPANDA
Mtu
mmoja mkazi wa kata ya Nsemulwa Wilayani Mpanda amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo
Mjini Mpanda kwa kosa la wizi wenye vitu vyenye thamani ya kiasi cha zaidi ya shilingi laki tatu.
Akisoma
shitaka hilo jana,mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi PC Mtei
mbele ya hakimu mwandamizi Bw.Davi Mbembela amesema mnamo tarehe 9 mei
majira ya saa 10 usiku mshtakiwa
Huseni Omary mwenye umri wa miaka
21 mkazi wa Nsemulwa aliiba mali ya Angel Helman mkazi wa kichangani.
Mtei
ameongeza kuwa alifanikiwa kuiba Godoro,shuka pamoja na fedha kiasi cha
shilingi laki moja na elfu sitini vyote vikiwa na jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi laki tatu.
Kwa
upande wake mshtakiwa amekana shitaka hilo
na mahakama imeahirisha shtaka hilo mpaka litakapotajwa tena tarehe 31
mei mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa tena na mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.
Mwandishi:Rogate Tweve
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments