SAUTI YA BUNGENI DODOMA KUHUSU HALMASHAURI YA WILAYA MPIMBWE MKOANI KATAVI
Serikali imesema kuwa imetenga kiasi
cha shilingi milioni 246 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara za Halmshauri ya
Wilaya ya Mpimbwe zenye urefu wa KM 42 kwa kiwango changalawe kwa mwaka wa
fedha 2015/2016.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri
wa Tawala za mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Mh.Suleiman Jafo,wakati
akijibu swali la mbunge wa jimbo la Kavuu Mh.Pudensiana Kikwembe aliyekuwa
akiuliza swali lililokuwa likihoji kuwa,serikali ina mpango gani na barabara
zilizopo katika Hamshauri Mpya ya Mpimbe ili kuondoa adha wanazozipata wananchi
wanapohitaji kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Aidha Waziri Jafo amesema kuwa katika
mwaka wa fedha 2016/2017 serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 324.3
zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara za changalawe zenye urefu wa KM
49.8 pamoja na matengenezo ya sehemu korofi katika Halmashauri hiyo.
Wakati huo Waziri Jafo akijibu swali
la nyongeza la Mh.Pudensiana Kikwembe ,pamoja na mambo mengine amesema kuwa Shilingi
bilioni zipatazo 45 zimetengwa katika kutengeneza maeneo korofi yanayounganisha
Halmshauri mbalimbali hapa nchini.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments