AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WIZI WA SIMU MPANDA
MTU mmoja amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo Mjini Mpanda
kwa Kosa la wizi wa simu zenye thamani ya shilingi laki tatu.
Akisoma
shitaka hilo hakimu mkazi wa mahakama hiyo
Mh,Sylvesta Makombe amemtaja mshtakiwa
kuwa ni Ally Wambura (23) mkazi wa Nsemulwa manispaa ya Mpanda.
Amesema
mshtakiwa ametenda kosa hilo mnamo Mei 2 mwaka huu maeneo ya Buzogwe ambapo
aliiba simu aina ya nokia na tecno pamoja na fedha taslimu kiasi cha shilingi
elfu hamsini ambazo ni mali ya Sara Kakoso mkazi wa Kawajense mjini Mpanda.
Hata hivyo
mshtakiwa amekana kutenda Kosa hilo ambapo Mahakama imeahirisha shtaka hilo
hadi litakapo tajwa tena Mei 30 mwaka huu kwa ajili ya kutoa hukumu.
Mwandishi :Rogathe Tweve
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments