WANAWAKE WANAOUZA MIILI YAO MPANDA WATAKIWA KUFIKA OFISI YA MKUU WA WILAYA KUPATA MBINU YA UJASILIAMALI KUEPUKA MAZINGIRA HATARISHI WALIYONAYO
WANAWAKE Wanaofanya biashara ya Kuuza
Miili yao Maarufu kama (Dada poa) Mjini
Mpanda wametakiwa Kufika Katika ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ili Wapatiwe Mbinu za Kuunda Vikundi
Vitakavyowawezesha Kuinua Uchumi ili kuwawezesha Kuachana na biashara hiyo.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Mh,Pazza Mwamlima wakati akizungumza na Mpanda fm ambapo amesema ofisi
yake iko tayari kuwasaidia kwa kuwapa Mikopo ili waachane na Biashara hiyo
ambayo Kisheria ni haramu.
Mh,Pazza
amesema endapo watakuwa tayari ofisi yake itawasaidia Kwa kuwapa Mafunzo ya
Ujasilia Mali kwa kuwatumia Maafisa Maendeleo ikiwa ni Pamoja na kuwapa Mikopo
ya Kufanyia biashara.
Uamuzi huo
wa Mkuu wa Wilaya umetokana na tukio la hivi Karibuni la baadhi ya Dada
poa Kuiomba Serikali Kuwapa leseni ya
Kuitambua Biashara yao ili Waisaidie Kukuza Uchumi wa Nchi kwa Kulipa Kodi Kama
Sehemu ya Kuunga Mkono Kauli ya Rais ya hapa Kazi tu.
Mwandishi:Meshack Ngumba
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea
kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments