HAKIMU MFAWIDHI MAHAKAMA YA WILAYA MPANDA ATOA WITO KWA WAKAZI MKOANI KATAVI KUEPUKA KUFANYA VITENDO UHARIFU
WANANCHI Mkoani Katavi wametakiwa kutofanya vitendo vya
uhalifu ili kuepuka madhara ambayo
yatapelekea kufungwa endapo watabainika na makosa.
Wito huo umetolewa na hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya
ya mpanda Bw.chiganga Tengwa wakati akizungumza na kipindi cha kumekucha Tanzania cha Mpanda Radio Fm mapema
hii leo.
Mh Chiganga amesema elimu ya kutosha inaendelea kutolewa kwa
wananchi kuhusiana na makosa na adhabu
zake ili kuweza kupunguza msongamano wa watu ambao wanafanya makosa mbalimbali.
Aidha amesema watu wengi wamekuwa wakipoteza haki zao za
msingi kutokana na kutojua sheria za nchi na kuwasihi wananchi kujua sheria
hizo kwani kwa kutofanya hivo ni kosa
kisheria.
Mwandishi:Meshack Ngumba
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments