SAUTI YA BUNGENI DODOMA KUHUSU MAKAZI MAPYA YA KATUMBA MKOANI KATAVI
Raia wapya
wa Tanzania wanaoishi Katika Makazi ya Katumba wanatarajia Kufanya Uchaguzi wa
Viongozi wa Serikali za Mitaa Mwaka huu
ikiwa Mandalizi yameanza Kufanyika.
Kauli hiyo
imetolewa na Naibu waziri ofisi ya rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Seleman Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Mh,Richard Mbogo
lililohoji ni lini Serikali itatenga fedha za Kukamilisha Uchaguzi wa Serikali
za Vijiji na Mitaa Katika Kambi ya Katumba ambayo sasa ni Makazi ya raia hao
wapya wa Tanzania.
Kwa Mjibu wa
Naibu waziri wa Tamisemi Katika Kata ya Katumba Kuna Vijiji 14 na Vitongoji 51
ambavyo havikufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2014.
Mh Jafo
amesema uchaguzi haukufanyika kwa sababu ya kuwepo kwa wakimbizi ambao walikuwa
hawajapewa uraia wa Tanzania kwa Mjibu wa Sheria za Nchi.
Ili
Kukamilisha Uchaguzi huo tayari serikali katika bajeti yake imetenga shilingi
Milioni 3.3 ilikuwezesha Uchaguzi huo Kufanyika.
Katika hatua
nyingine Mbunge Mbunge wa Nsimbo Richard Philip Mbogo amehoji zaidi ni kwa
namna gani Serikali itashirikiana na Shirika la Wakimbizi Duniani UNHCR katika
kutatua chanamoto za elimu,maji na barabara zinazowakabili wakazi wa makazi
hayo ambapo serikali imesema kuwa inaendelea
na utarartibu kupanga utaratibu wa kuwasiadia.
Wakati huo
huo mbunge viti maalumu jimbo la ULYAKULU Mh.Mwaine Jumanne akauliza kuwa kwa
kuwa tatizo lililopo la kutofanyika kwa uchaguzi Katumba ni sawa na lililopo
jimboni kwake Ulyankulu,ni lini uchaguzi utafanyika,swali hili pia likijbiwa na
Naibu waziri ofisi ya rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jafo
amesema kuwa mchakato utaendelea wa maandalizi ya uchaguzi katika kata 3
zilizosalia baada ya eneo hilo kurudishwa katika mamlaka ya TAMISEMI kwa kuwa
sasa mmiliki wa eneo hilo yupo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments