WANAKIJIJI KASOKOLA MKOANI KATAVI WAKATAA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI,KUSOMWA UPYA MEI 12 MWAKA HUU.
Wananchi
wa kijiji cha kasokola kata ya kasokola manispaa ya mpanda wameikataa taarifa
ya mapato na matumizi iliyosomwa katika
mkutano wa hadhara ambapo haijasomwa takribani mwaka mmoja na miezi mine.
Wananchi
hao wamesema kuwa taarifa hiyo ina mapungufu mengi ikiwemo baadhi ya michango
kutoingizwa katika taarifa hiyo hali ambayo imepelekeaa sintofahamu baina ya
wananchi na viongozi waliohusika katika kuandaa taarifa hiyo.
Hali
hiyo imepelekea mkutano huo kuahirishwa hadi may 12 kutokana na baadhi ya
wajumbe wa serikali ya kijiji hicho ambao ndiyo waliohusika kuandaa taarifa
hiyo kutohudhuria mkutano huo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho cha
kasokola Bw. Dominic Fungameza amesema yeye hahusiki na tuhuma hizo za
ubadhilifu wa fedha za wananchi.
Mwandishi: Judica Schone
Mhariri ;Issack Gerald
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments