WALIMU WAGOMA KUFUNDISHA WAKIPINGA MWALIMU MWENZAO KUPIGWA NA AFISA ELIMU,CWT KUTOA TAMKO LEO
WALIMU wa shule ya msingi Kianda wameanza mgomo wa siku mbili
wa kutofundisha shuleni hapo huku wakilaani kitendo cha Ofisa Elimu (Shule za
Msingi) wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Peter Fusi
kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani mbele ya
wanafunzi wake.
Makamu Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Flora Kipesha alisema
wameitisha mgomo huo wa siku mbili kupinga kitendo cha Fusi kumshambulia na
kumpiga makofi mwalimu mwenzao Jacob Msengezi (25) ambaye anafundisha somo la
Hisabati Darasa la Saba shuleni hapo.
Akifafanua,alisema walimu hawataingia kufundisha kwa siku
hizo mbili na watakuwa ofisini wakiandaa mitihani huku wanafunzi wakiendelea
kuhudhuria shuleni hapo kama kawaida.
Naye Mwalimu Msengezi aliliambia gazeti la Habari leo kwa akiwa
shuleni Kianda kuwa juzi Jumatano Ofisa Elimu, Fusi alitembelea shuleni hapo saa
tatu asubuhi akikagua mazingira ya shule na hatimaye kufanya kitendo hicho.
Katibu wa CWT Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Vicent Ndewele amekiri
kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza kuwa chama hicho kitatoa msimamo wake
leo.
Comments