BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA MPANDA USIKU WA KUAMKIA LEO MEI 21,LAPITISHA WATUMISHI 13 KATI YA 16 WALIOKUWA WAMESIMAMISHWA KAZI KUKATWA MISHAHARA KUFIDIA HASARA ILIYOTOKANA NA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA MIRADI ZA MANISPAA,MMOJA AFUKUZWA KAZI,WENGINE WATUPIWA TAMISEMI IWAPANGIE INAKOTAKA MBALI NA MANISPAA
Baraza la madiwani katika Manispaa ya
Mpanda Mkoani Katavi ,limepitisha maamuzi
ya kukata mshahara wa watumishi 13 kati ya 16,waliokuwa wamesimamishwa
kazi na baraza hiloFebruari 26 mwaka huu,kutokana na tuhuma mbalimbali zikiwemo
utumiaji ovyo wa fedha za manunuzi ya gari la kuzoa taka pamoja na ubadhilifu
wa fedha ya skimu ya umwagiliaji maji ya kakese ambapo pia watumishi watatu
wameshushwa vyeo.
Uamuzi wa baraza hilo umetolewa usiku
wa kuamkia leo Mei 21,2016 katika kikao maalumu ambacho kimefanyika katika
ukumbi wa Manispaa ya Mpanda na kuhudhuriwa na wajumbe,watendaji na wataalamu
wakuu wa idara zaidi ya 120.
Akitangaza maamuzi ya baraza hilo
yaliyotokana matokeo ya tume iliyoundwa
kuchunguza tuhuma za watumishi hao Februari 26 mwaka huu,Mstahiki Meya wa
Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda Mh.Willium Philip Mbogo ambaye pia ni diwani
wa kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda,amewataja watumishi watakaokatwa
mishahara ili kufidia hasara iliyotokana na makosa waliyoyafanya kuwa ni pamoja
na Charles Ngonyani mkuu wa idara ya ushirika,chakula na umwagiliaji, Brian
Severe mkuu wa idara ya ardhi,mipango miji na maliasili, Vicent Kayombo mkuu wa
idara ya elimu Shule ya Msingi, Abrahamu Kaswa afisa mipango miji, Paschal
Kweya afisa afya Mazingira Manispaa ya Mpanda, Gerigori Lugarema afisa
maendeleo ya jamii msaidizi.
Wengine amewataja kuwa ni Bw.Gorge
Ngongolowo mhasibu mwandamizi, Albert Kiando mhandisi wa ujenzi, Victa
Lutajumulwa mwalimu Mkuu elimu ya msingi daraja la pili, Focus Bilamule mhasibu
Manispaa ya Mpanda, Jefu Julius mhandisi
umwagiliaji Manispaa, Said Mandua Afisa mazingira wa Manispaa ya
Mpanda,Bw.Fredinandi Filimbi Mkuu wa idara sera na ufuatiliaji aliyekuwa
ameshamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo alirejeshwa Manispaa
Mpanda baada ya tuhuma.
Aidha Mh.Mbogo aliwataja walioshushwa
vyeo kuwa ni Bw.Chamilius Luhinda Kaimu mkuu wa kitengo cha sheria
Manispaa,Kibi Hamis Musaka Mhasibu Mwandamizi-Mhasibu mfumo wa EPICA ambapo pia
yeye baraza limeamua atafutiwe kituo kingine cha kazi sawa na Bw.Bosko Kapinga
mweka hazina wa Manispaa ambaye pia ameshushwa cheo huku baraza likiendelea
kuwasiliana na mamlaka husika(TAMISEMI) ili aondolewe katika Manispaa ya Mpanda
na kuhamishhiwa nje ya Manispaa.
Wakati huo huo baraza limesema kuwa
haliwezi kutoa maamuzi ya kesi ya aliyekuwa Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda
Bw.Suleiman Lukanga anayedaiwa kutapanya zaidi ya milioni 380 katika miradi
yote ya gari hewa na skimu ya umwagiliaji Kakese,kutokana na sheria kuelekeza
kuwa maamuzi juu ya Mkurugenzi yanatolewa na katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI
Ofisi ya Rais.
Mtumishi Mwingine ambaye baraza
halikutoa maamuzi ni juu ya Bi.Vumilia Kakulima mkuu wa kitengo cha Manunuzi
kutokana na mashauri ya tuhuma hizo kuwa tayari zipo mahakamani ambapo baraza
limesema linasubiri maamuzi ya mahakama ili sheria zichukuliwe dhidi yake.
Katika hatua nyingine,Frenk Gombanila
aliyekuwa ameajiriwa kama Mhudumu idara ya afya Manispaa ya Mpanda anyeadiwa
kughushi vyeti na kupata ajira,amefukuzwa kazi pamoja na Shauri lake lipo kupelekwa
Polisi ambapo pamoja na hali hiyo alikuwa miongoni mwa watumishi hewa Manispaa
ya Mpanda.
Wakati huo huo,Yusra Marco Mtunza
Kumbukumbu aliyekuwa na shtaka la utoro na hivyo kuonekana kuwa mtumishi hewa
amerejeshwa kazini kutokana na kutokuwa na hatia kwa kuwa makosa yalifanyika
akiwa hayupo.
Hata hivyo Mstahiki Meya Mh.Mbogo
amesema kuwa ikiwa mtumishi yeyote hataridhika
na maamuzi ya baraza la madiwani anaruhusiwa kukataa rufaa.
Watumishi waliokuwa wakikaimu nafasi
za waliokuwa wamesimamishwa kazi kuanzia Februari 26 mwaka huu walikuwa ni Said
Mohamed Hemed mkuu wa idara ya ushirika,chakula na umwagiliaji,Rashid Pili
Idara ya elimu Msingi,Mabokera Mwakabamba kitengo cha Manunuzi,Paschal Sindani
idara ya ujenzi,Juma Luhomwa mweka hazina wa Manispaa huku Peter Charles Mkalipa atakaimu mkuu wa
idara,ardhi na maliasili.
Hata hivyo katika mjadala wa nadalaza
la madiwani uliodumu kwa siku mbili mfululizo usiku na mchan,takwimu kamili ya
hasara iliyokana na watumishi kufanya ubadhirifu huo haijatajwa mbali na zaidi
ya milioni 380 zilizokuwa zimetajwa katika mradi wa Skimu ya umwagiliaji Kakese
pamoja na ununuzi hewa wa gari la kuzoa taka .
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao
hicho maalumu wamesema kuwa ikiwa pesa yote itarudishwa huenda ikapatikana pesa
ya kutosha kuendesha miradi ya mendeleo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
pekee
Comments