DUKA LATEKETEA KWA MOTO MPANDA,ZIMAMOTO WAENDELEA NA UCHUNGUZI WA CHANZO
DUKA
moja limeteketea kwa moto na kuungua baadhi ya bidhaa zilizokuwemo ndani katika
maeneo ya soko la Mpanda hoteli mkoani Katavi.
Wakizungumza
baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema moto huo umetokea majira ya saa tatu
usiku ambapo hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.
Kwa
upande wake kaimu kamanda wa kikosi cha zimamoto mkoa wa katavi Bw.Nestory
Konongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema bado uchunguzi
unaendelea ili kubaini chanzo chake.
Aidha
ametoa wito kwa wafanyabiashara kuhudhuri semina zinazotolewa na kikosi hicho
ambapo amewashauri kuwa na mitungi ya kuzimia moto katika maeneo yao ya
biashara.
Katika
2016 ajali ya moto siyo ya kwanza,ambapoi mapema mwezi Februari shule moja ya
sekondari nayo bweni moja la wavulana lake liliteketea katika Manispaa ya
Mpanda.
Mwandishi:Rogate Tweve
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM pekee
Comments