ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 3 KUTUMIKA KUJENGA HOSPITALI YA MKOA WA KATAVI
SERIKALI
ya mkoani katavi imeazimia kutumia kiasi
cha zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa ajili ya
kuanzisha ujenzi wa hospitali ya mkoa.
Hayo
yamebainishwa jana na mkuu wa mkoa wa katavi meja jeneral Raphael Muhuga wakati
akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya maridadi manispaa ya
Mpanda.
Muhuga
amesema kuwa haospitali ya wilaya ya
Mpanda haitoshi ukilinganisha na
mahitaji ya watu ambapo katika vikao vya
bajeti imepewa kipaumbele.
Aidha
amesema vituo vya afya vitaboreshwa ambavyo viko nje ya manispaa ili kupunguza
msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya.
Kwa sasa Hospitali ya Wilaya ya
Mpanda inatoa huduma kwa wakazi wote Mkoani Katavi ikibeba jukumu kama
Hospitali ya Mkoa ambapo changamoto kubwa ambazo zimekuwa zikiibuka katika
hospitali hiyo ni msongamano wa wagonjwa usioendana na miundombinu na upungufu
wa dawa na vifaa tiba.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA MEDIA
Comments