AHUKUMIWA JERA MIEZI 6 KWA KOSA LA WIZI MPANDA
Mahakama ya
mwanzo mjini Mpanda imemhukumu mtu mmoja mkazi wa Nsemlwa kifungo cha miezi 6
jera au kulipa faini kiasi cha shilingi laki mbili na nusu kwa kosa la wizi kinyume na kifungu cha
sheria namba 265 sura 16 kanuni ya adhabu.
Akisoma
hukumu hakimu mkazi wa mahakama hiyo mh, Sylivesta Makombe amemtaja bw,Ally Mtaragulwa (23) mkazi wa
Nsemulwa kuwa mnamo mei 2mwaka huu
majira ya saa 2na dakika 45 asubuhi aliiba cm mbili aina ya nokia na
tekno zenye thamani ya shilingi laki tatu mali ya Sara Kaposwe mkazi wa
kawajense.
Mshitakiwa
alipopewa nafasi ya kujitetea ameiomba mahakama impunguzie adhabu kwani hahusiki
na wizi wa sm hizo ametakiwa kurudisha gharama za sm alizoiba .
Wakati huo
kesi inayomkabili mchungaji wa kanisa la Moravian kwa tuhuma za meno ya tembo
kukutwa katika ofisi ya kanisa lake jana imeendelea kusikilizwa na hatimaye
kuahirishwa baada ya upande wa mashahidi wa mshtakiwa kudai kupewa nafasi ya
kukusanya ushahidi zaidi.
Mwandishi : Vumilia Abel
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments