WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI
WATU wawili wakazi wa Makanyagio wamefikishwa katika
mahakama ya wilaya ya Mpanda kwa kosa la ubakaji.
Akisoma shitaka hilo jana katika hatua ya ushahidi mwendesha
mashtaka wa jeshi la polisi PC .Pelepetua mbele ya hakimu mfawidhi Mh.Chigangwa
Tengwa amewataja washitakiwa kuwa ni
Peter Samson (32) na Dotto Peter(38)
wote wakazi wa Makanyagio Manispaa ya Mpanda .
Imedaiwa kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo desemba
08, 2015 katika nyumba ya kulala wageni maarufu kama Visiwa Guest house.
Kufuatia hatua hiyo mahakama imeahirisha shitaka hilo
hadi itakapo tajwa tena
juni 13 mwaka huu.
Mwandishi : Vumilia Abel
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments