MBUNGE JIMBO LA MPANDA VIJIJINI ALINDIMA BUNGENI DODOMA KUTETEA VITUO VYA AFYA JIMBONI KWAKE
VITUO
vya afya vya Mwese,Karema na Mishamo Wilayani Mpanda Vinakabiliwa na ukosefu wa
wataalaamu wa afya na gari la wagonjwa-leo Mbunge Jimbo la Mpanda Vijijini
Mh.Suleiman Kakoso alindima bungeni kutetea vituo hivyo.
Hali
hiyo imeibuka wazi leo kufuatia Swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa
jimbo la Mpanda vijijini Bw Suleiman Kakoso lililo hoji je ni lini serikali itavipatia mahitaji hayo vituo hivyo ili kuokoa maisha
ya wananchi.
Akijibu
swali hilo waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI Bw George Simba Chawene amesema serikali
kwa sasa haina mpango mahususi wa kununua magari ya wagonjwa kwa nchi nzima isipokuwa wanangalia bajeti ya
halimashauli zao.
Aidha
Chawene amesema sehemu ya kuanzia kukamilisha huduma mbambali katika sekta za
elimu pamoja na afya mipango hiyo huanzia katika halmashauli.
Mbali
na chanamoto hizo katika vituo hivyo,pia vituo hivyo na vinginevyo katika jimbo
hilo vimekuwa vina matatizo ya ukosefu wa huduma ya maji ya uhakika kikiwemo
kituo cha afya cha Mwese.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments