WANANCHI WILAYANI MLELE WATAKIWA KUWA MABALOZI WA MFUKO WA BIMA YA AFYA WA CHF
WANANCHI
katika kata ya Ilunde Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani katavi wametakiwa
kuwa mabalozi katika maeneo mbalimbali katika uhamasishaji wa wananchi kujiunga
na mfuko wa jamii wa bima ya afya CHF.
Rai
hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya mlele Godwini
Beene wakati wa zoezi la uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa jamii wa
bima ya afya CHF yaliyofanyika katika ofisi za kata ya ilunde wilayani humo.
Kwa
upande wake meneja wa mfuko huo katika mkoa wa katavi Dk. Clement Massanja lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo ni kusaidia
kaya kupata huduma bila malipo kwa kuchangia kiasi cha shilingi elf 10 kwa
mwaka na kuwataka wananchi kuuamini mfuko huo kwani ndiyo mkombozi wao.
Katika
zoezi hilo zaidi ya kaya 40 zimejiunga na mfuko huo hali ambayo inazidi kuiweka
kata hiyo katika nafasi nzuri ya wananchi kujiunga na mfuko huo katika
halmashauri hiyo.
Mwandishi : Judica Schone
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA
MEDIA
Comments