HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imezindua Mnada mpya wa mifugo
wa Bulamata uliopo kata ya Bulamata ambapo pia bidhaa tofauti na mifugo
zinatarajiwa kuuzwa katika mnada huo.
|
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Hassan Mapengo akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata (PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) |
|
Afisa Mifugo Halmshjauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elikana Magambo akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Bulamata na maeneo jirani wakati wa uzinduzi wa Mnada wa Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) |
|
Ng'ombe wakiwa mnadani siku ya uzinduzi wa a wa BulamataMnad(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) |
|
Mmoja wa wapishi katika mnada wa Bulamata siku ya Uzinduzi(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) |
|
Mama akitengeneza kitoweo cha wateja katika mnada wa Bulamata siku ya Uzinduzi(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) |
|
Baadhi ya wafanyabiasahara wadogo katika mnada wa Bulamata siku ya Uzinduzi(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) |
|
Afisa Mifugo Halmshjauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elikana Magambo akitoa taarifa ya Mnada wa Bulamata wakati wa
uzinduzi wa Mnada wa Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) |
|
Mh.Augustino Sadick Mathew diwani wa kata ya Ilangu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata (PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) |
|
Mh.Sikudhani Kolongo diwani viti maalumu diwani kata ya Mishamo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata (PICHA NA.Issack Gerald Mei 10,2016) |
|
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Hassan Mapengo
akihutubia wakazi wa kijiji cha Bulamata wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata (PICHA NA.Issack
Gerald Mei 10,2016) |
|
Viongozi na wanakijiji cha Bulamata wakati wa uzinduzi mnada wa Bulamata(PICHA NA.Issack
Gerald Mei 10,2016) |
|
Mbuzi akiwa katika mnada wa Bulamata aliyeletwa kuuzwa (PICHA NA.Issack
Gerald Mei 10,2016) |
|
Afisa mtendaji kijiji cha Bulamata Bw.Joseph Lusambo akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Mh.Hamad Mapengo wakati wa uzinduzi wa mnada wa Bulamata(PICHA NA.Issack
Gerald Mei 10,2016) |
Akizindua mnada huo,mwenyekiti wa
Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Mapengo,amewataka wafanyabiashara
watakoatumia mnada huo kuutumia vizuri kwa ajili ya maendeleo.
Kwa upande wake Afisa mifugo
Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elikana Magambo ametoa wito kwa
wafanyabiasahara hasa wa mifugo kuzingatia kibali cha kuuza mifugo kutoka
mamlaka husika ili kuthibitisha uhalali wa mifugo wanayotaka kuuza.
Wakati huo huo wakizungumza kuhusu
usalama mnadani hapo,afisa mifugo Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elikana
Magambo na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Mapengo wametoa wito kwa vyombo vya
usalama hususani kata za Bulamata na Mishamo kuhakikisha usalama wa kutosha unakuwepo
ili kuzuia wizi wa mali na fedha za wafanyabiashara.
Awali akisoma taarifa ya mnada
huo,Afisa mtendaji kwa kijiji cha Bulamata Bw.Joseph Lusambo,amesema kuwa
asilimia 85 ya wakazi wa kata ya Mishamo iliyogawanyika na kupata kijiji na
kata ya Bulamata,wanajihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji ambapo pia
amesema,kwa mjibu wa sensa ya wanayama iliyofanywa na chama cha wafugaji kijijini hapo kwa mwaka
2012,ni pamoja na ng’ombe 19630,mbuzi 12,912, kondoo 273,ngururuwe 264,kuku
27491,bata 2126,mbwa 612,punda 61 na paka 465.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo
msaidizi wa polisi kituo cha Mishamo,Afande Julius Chemka amesema kuwa
wamejipanga kuhakikisha usalama wa kutosha unakuwepo siku za mnada.
Mmoja wa wananchi walikuwepo katika
uzinduzi wa mnada wa Bulamata Bw.Wambura Ernest amesema anatarajia kuuza
biashara yake kwa mafanikio kutokana na watu wengi kufika katika mnada huo
kununua bidhaa mbalimbali.
Mnada huo wenye ukubwa wa ekari 100
unatarajia kuwanufaisha watu wapatao 6000 wanaozunguka eneo la mnada suala
ambalo limepongezwa na wakazi wa kijiji cha Bulamata pamoja na viongozi
mbalimbali wakiwemo Mh.Frenk Kibigas diwani kata ya Tongwe,Mh.Augustino Sadick
Mathew diwani kata ya Ilangu,Mh.Rehani Simba diwani wa Kata ya Ipwaga ,Mh.Sikudhani
Kolongo diwani viti maalumu kata ya mishamo na diwani wa kata ya Bulamata.
Afisa Mifugo wa Halmshauri ya Wilay
aya Mpanda Bw.Elikana Magambo amesema,kuzinduliwa kwa mnada wa
Bulamata,kunakamilisha jumla ya minada 5 inayoiingizia kipato Hamshauri ya
Wilaya ya Mpanda ambapo minada hiyo ni Sibwesa,Kapanga,Kapalamsenga,Mnyagala na
Bulamata ambapo.
Halikadhalika magulio matatu ya Mwese,Vikonge
na Ilebula yametajwa kuwa ni miongoni mwa vyanzo vya mapato vya Halmshauri ya
Wilaya ya Mpanda.
Mnada huo utakuwa unafanya kazi
tarehe 10,11 na 28 ya kila mwezi.
Mwandishi : Issack Gerald
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika
na P5 TANZANIA MEDIA
Comments