RIPOTI KAMILI YA TAKUKURU MKOANI KATAVI KUWABULUZA MAHAKAMANI WATU WATATU KATI YA WATANO HII HAPA
TAASISI
ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Katavi TAKUKURU imewafikisha watu
watatu katika mahakama ya wilaya ya
Mpanda kwa kosa la uhujumu uchumi.
Watu
hao walifikishwa mahakamani kwa kukabiliwa na mashitaka matatu ambayo ni ya kutumia nyaraka na kumdanganya mwajiri,kutumia madaraka
vibaya na kuisababishia serikari hasara ya zaidi ya shilingi milioni 61,159.40.
Mawakili
na wanasheria wa Takukuru Mkoani Katavi Bw.Bahati Stafu Haule na Simon Buchwa
waliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Naomi
Ndelelio Nnko Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambaye pia
aliwahi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda,Godfrey Athanase Majuto ambaye ni Mhandisi Mjenzi Halmshauri ya Manispaa ya Songea
ambapo pia katika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda alikuwa ni Mhandisi
Mkuu kitengo cha ujenzi.
Watuhumiwa
wengine ni Beatus Joseph Bisesa Mhandisi Ujenzi ya Ukandarasi ya Matoke
Constraction Caompany na Mmiliki wa Kampuni hiyo ya Ukandarasi Mhandisi Chiyando Muyenjwa Matoke ambaye kwa
sasa ni Mhandisi ujenzi Halmshauri ya Wilaya ya Kishapu pamoja na Petro Jurgen Mwanoni aliyekuwa Mhandisi
Mchundo wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda.
Wakisomewa
shitaka hilo na mawakilii pamoja na wanasheria wa Taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani Katavi mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Chiganga Tengwa,washitakiwa
hao walikana kosa.
Mawakili
na wanasheria hao waliiambia mahakama kuwa mnamo Tarehe 15/11/2012,Ofisi ya
TAKUKURU mkoani Katavi ilifanya ilipokea taarifa iliyotuhumu kuwa kumekuwa na
ukiukwaji wa wa taratibu katika kutekeleza mradi wa barabara ya Kasokola-Mtapenda-Nsemulwa
yenye urefu wa KM 22 wakituhmu kuwa Ofisi ya Mkurugenzi Halmshauri ya Wilaya ya
Mpanda imezembea kusimamia mradi huo kwani Kampuni au mkandarasi ameshindwa
kufanya kazi hiyo na badala yake kufanywa na kampuni au mkandarasi mwingine
tofautikinyume na mkataba ambapo hata hivyo matengenezo ya barabara hiyo
haikukidhi kiwango kutokana na fedha iliyokuwa imekwishakulipwa.
Aidha
TAKUKURU mkoa wa katavi imetoa wito kwa
wanachi wote Mkoani Katavi kujiepusha na vitendo vya rushwa katika sekta za
umma na za watu binafsi.
Washtakiwa
watatu waliokuwepo mahakamani,wawili kati yao walikidhi vigezo vya masharti ya
dhamana yaliyowekwa na mahakama ambao ni Naomi Ndelelio Nnko na Godfrey
Athanase Majuto huku Chiyando Muyenjwa Matoke akiwekwa mahabusu hadi
atakapotekeleza masharti ya dhamana hiyo.
Hata
hivyo Watuhumiwa wote walikana mashtaka dhidi yao.
Mwandishi
: Issack Gerald
Mhariri
: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5
TANZANIA MEDIA
Comments