IDADI YA WATUMISHI HEWA YAZIDI KUPANDA KATAVI KUTOA 21 MWEZI ULIPOITA SASA 46 SERIKALI YAPATA HASARA ZAIDI YA MILIONI 200,MKUU WA MKOA WA KATAVI ATOA SIKU SABA KWA MKURUGENZI KUWAFUKUZA KAZI WATUMISHI HEWA
IDADI ya Watumishi hewa Mkoani Katavi
imeongezeka Kutoka 21 ya awali na kufikia watumishi hewa 46 walioisababishia
Serikali hasara ya Shilingi Milioni 200,792,448.
Meja
Jenerali Muhuga amesema Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ambayo awali haikuwa
na watumishi hewa imeongoza kwa kuwa na idadi ya watumishi hewa 16
walioisababishia Serikali hasara ya shilingi Milioni 31,231,516.
Aidha
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambayo awali ilikuwa na watumishi hewa 17
Imeshika nafasi ya pili kwa kuwa na Watumishi hewa 11 Walioisababishia Serikali
hasara ya Shilingi Milioni 90,641,880.
Mkuu
wa Mkoa amesema kuwa Katika Mkoa wa Katavi, watumishi waliokufa wanaoendelea kulipwa mishahara ni 5,Waliostaafu ni 19,walioacha
kazi kwa hiari 1,waliokuwa na mishara
miwili -2,Watoro Sugu ambao
hawapo vituoni 13, vyeti vya kughushi
ambao baada ya timu kuanza uchunguzi walitokomea kusikojulikana 3 na waliofukuzwa ni 3.
Katika
Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi mpaka sasa,Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
imeonekana kuongoza kwa kuwa na watumishi hewa 17 kutoka 9 Machi 30 mwaka huu
na kuisababishia serikali kupata hasara ya Shilingi Mil.31,231,516/=,ikifuatiwa
na Manispaa ya Mpanda yenye watumishi hewa 16 walioisababishia serikali hasara
ya shilingi Mil.90,641,880 ambapo katika Ripoti ya Aprili 21 mwaka huu ilisema
kuwa haikuwa na mtumishi hewa hata mmoja,Mlele ina watumishi hewa 10 kuotoka 2
machi 31 ambapo hiyo ni sawa na hasara ya Shilingi Mil.45,650,900/=huku
Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda ikiwa na watumishi hewa 09 walioisababishia
hasara ya shilingi Mil.33,268,152 na kufanya JUMLA KUU ya hasara ya fedha za serikali katika Mkoa wa Katavi kuwa
MIL.200,792,448
Hata
hivyo pamoja na kuishukuru timu kwa uchunguzi mzurzi,Mkuu wa Mkoa ametoa siku
21 kwa wakurugenzi wa halmashauri zote Mkoani Katavi kuhakikisha fedha zote
zinarudishwa huku akitoa siku 7 kwa wakurugenzi hao kufuta watumishi hewa wote.
Mwandishi
:Meshack Ngumba
Mhariri
:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments