VIKUNDI 4 KATI YA 28 VYA WAJASILIAMALIVILIVYOPO KATA YA NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI VIMEKABIDHIWA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 1 KUTOKA MFUKO WA JIMBO WA MBUNGE WA JIMBO LA MPANDA MJINI.
Vikundi 4 kati ya 28 vya
wajasiliamali vilivyopo kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,leo
vimekabidhiwa mkopo kwa Shilingi milioni Moja kwa ajili kufanya shughuli za
kujikwamua kiuchumi.
Akikabidhi hundi ya fedha hiyo katika
mkutano wa viongozi na wajasiliamali hao,Diwani wa kata hiyo Mh.Bakari Kapona
amevitaka vikundi hivyo kutumia fedha hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Afisa mtendaji wa
Katavi hiyo Bw.Jumbe Museluka amesema kuwa kila kikundi kimepata Shilingi laki
mbili na nusu ambapo amewataka kuzirejesha fedha hizo kwa wakati ili vikundi
vingine vipatiwe mkopo huo kila baada ya miezi mitatu.
Wakizungumza kwa niaba ya wanachama
wenzao,viongozi wa vikundi hivyo pamoja na mambo mengine,wametoa shukrani kwa
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Mh.Sebastian Kapufi kwa kuendelea kutekeleza
ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi kwa mwaka 2015.
Makabidhiano hayo ambayo yamefanyika
katika Ofisi za Kata ya Nsemulwa zimehudhuriwa na Adam Masigati Mwenyekiti wa
mtaa wa Nsemulwa,Emmanuel Luhamba mwenyekiti wa mtaa Kilimahewa
Nsemulwa,Revocatus Pekewe wa mtaa wa Kichangani,Ahamad Kahena Makokolo sanjari
na viongozi wa chama cha Mapinduzi ambapo Kwa upande wake Christopher Simon Watujabo
ambaye ni msemaji wa chama cha Mapinduzi CCM katika Kata ya Nsemulwa akisema
kuwa hueo ni mwendelezo wa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi
inayofanywa na Mbunge Mh.Sebastian Kapufi pamoja na kuupongeza uongozi wa kata
ya Nsemulwa kwa kuviandaa vikundi.
Shughuli mbalimbali ambazo zimeelezwa
kufanywa na vikundi mbalimbali vya wajasiliamali katika Mkoa wa Katavi ni
pamoja na ufugaji wa kuku,biashara ndogondogo,kilimo ambapo wajasiliamali wa
kata ya Nsemulwa walio wengi wameelezea kuhakikisha wanaondokana na ukali wa
maisha kwa kutumia pesa kwa malengo yaliyokusudiwa huku wakisisitiza kuwa
makini na baba wa familia kuzitumia fedha hizo kwa ajili ya ulevi.
Vikundi hivyo ni San Vela Group cha
Kilimahewa,Smathday cha Nsemulwa,Iyombabuzoba cha Migazini na Ilakoze Group cha
Mtaa wa Nsemulwa.
Mwandishi: Issack Gerald
Mhariri ;Issack Gerald
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments