MKURUGENZI MANISPAA YA MPANDA APEWA SIKU 14 NA MKUU WA WILAYA YA MPANDA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI MISUNKUMILO
MKUU wa wilaya ya Mpanda Mh,Paza Mwamlima ametoa
siku 14 Kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Kutatua Mgogoro wa
aridhi kwa wananchi wa kata ya Minsunkumilo.
Mh,Paza Mwamlima ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na Baadhi ya wakazi wa
kata hiyo Katika Kikao cha Kutafuta suluhu ya Mgogoro huo Kilichofanyika Katika
Ukumbi wa Idara ya Maji Mjini Mpanda.
Kwa
upande wake kaimu afisa ardhi manispaa ya mpamba Bw. Peter kalipa amesema kwa
mtu yeyote ambae atakuwa na vielelezo
vinavyoonesha kuwa ni muhusika wa eneo hilo afike katika idara hiyo ili
aweze kusaidiwa.
Mkoa
wa Katavi ni miongoni mwa Mikoa hapa nchini yenye Migogoro ya aridhi hasa
Maeneo ya Vijijini inayotokana na wananchi wengi Kutokuwa na elimu inayohusu
Masuala ya aridhi.
Mwandishi :Vumilia Abel
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments