BODI YA CHAMA CHA MSINGI CHA USHIRIKA MPANDA KATI YAVUNJWA
BODI ya chama cha msingi cha ushirika cha wakulima wa tumbaku
maarufu kama Mpanda Kati imevunjwa.
Taarifa ya kuvunjwa kwa bodi hiyo,imesomwa na Mkaguzi watume
ya maendeleo hapa nchini Bw.Eliah Richard mbele ya wanachama wa chama hicho ambapo
awali aliwataka wakulima hao kuwa na utulivu.
Pamoja na mambo mengine,amesema adhabu mbali mbali
zitakazochukuliwa dhidi ya viongozi waliotuhumiwa kutapanya fedha za wakulima kuwa
zitatolewa kwa mujibu wa sheria za vyama vya ushirika nchini na kwamba vyombo
vya sheria vitaendelea kuchukua hatua kwa wote walio patikana na hatia kufuatia
uchunguzi uliofanywa na tume hiyo.
Hata hivyo,baadhi ya wakulima wamelezea kutokuridhishwa na
baadhi vipengele vya hatua zilizochukuliwa kwa madai kuwa huenda usipatikane
mwarobaini wa tatizo litakalotibu madai yao.
Januari 11,2016, Naibu waziri wa kilimo,mifugo na Uvuvi Mh.Tate
Ole Nasha akiwa Mkoani Katavi kusikiliza kero za wakulima wa zao la
tumbaku,alimwagiza mrajisi wa vyama vya ushirika hapa nchini kuunda timu ya
uchunguzi na ukaguzi wa malalamiko ya wakulima waliokuwa wakilalamika fedha zao
takribani milioni 600 walizodai kuwa zilikuwa zao zilizotokana na zao la tumbaku
kuliwa na viongozi wa chama cha ushirika.
Wakati huo huo walidai kuwa Chama kikuu cha ushirika LATCU
kimekuwa hakitetei maslahi ya wakulima wa tumbaku na badala yake kimekuwa
kikiwadidimiza na kujikuta wakiendelea kuwa katika dimbwi la umaskini.
Mwandishi:Alinanuswe Edward.
Mhariri :Issack Gerald
Bathromeo
Endelea kuwa na P5 TANZANIA MEDIA
Comments