DIWANI KATA YA KATUMBA WILAYANI MPANDA KIZIMBANI KWA RUSHWA YA ZAIDI YA SHILINGI MIL.1
TAASISI ya Kuzuia na
kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Katavi imemfikisha kizimbani diwani wa kata ya Katumba kwa kosa la kujihususha na vitendo vya
rushwa.
Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya
wilaya ya Mpanda Bw Chiganga Tengwa mwendesha mashtaka wa TAKUKURU mkoa wa katavi Simon Buchwa amemtaja shtakiwa kuwa ni Seneta Baraka (30)
ambaye ni diwani wa kata ya katumba.
Inadaiwa kuwa mnamo tarehe
12 mei mwaka huu mshtakiwa aliomba rushwa kiasi cha shilingi milioni moja kwa Charles Msukuma mkazi wa ivanga kata ya
Katumba ambayo ilihusiana na kumuondolea
tuhuma katika mahakama ya mwanzo ya Katumba ambapo anatakiwa aondoke na mifugo
yake katika makazi ya wakimbizi.
Na wakati huohuo mei 12
mwaka huu pia amedaiwa kuomba rushwa kiasi cha shilingi laki nne kutoka kwa
huyohuyo Charles msukuma ikiwa ni ushawishi wa kumuondolea mifugo katika makazi ya hifadhi ya wakimbizi kata ya Katumba.
Kufuatia hatua hiyo
mshtakiwa amekana kosa na kupelekwa lumande kwa kukosa
kukidhi vigezo vya dhamana ambapo mahakama imeahirisha shtaka hilo hadi
litakapotajwa tena mei 31 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.
Hiyo siyo mara ya
kwanza viongozi wa umma kufikishwa mahakamani kwa vitendo vya kuomba na kupokea
rushwa ambapo kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2016 vigogo wa serikali akiwemo
mwanasheria mkuu wa Mkoa wa Katavi walifikishwa mahakamani kwa vitendo vya
rushwa
Mwandishi:Mgeni
Shabani
Mhariri:Issack
Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOSPOT.COM
Comments