RIPOTI KAMILI YA TUHUMA ZA MENO YA TEMBO: MCHUNGAJI KANISA LA MORAVIAN WILAYANI MLELE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKAMATWA NA MENO YA TEMBO YENYE ZAIDI YA SHILINGI MIL.90
MCHUNGAJI
wa kanisa la Moravian wilaya ya mlele
mkoni Katavi Gonweli Siame amefikishwa mahakamani katika mahakama ya
hakimu mkazi mkoa wa katavi kwa kosa la
uhujumu uchumi kwa kukutwa na meno ya tembo yenye thamani zaidi ya million 90.
Akisoma
sahitaka hilo hakimu mfawidhi Tigagwa Tengwa wakili wa serikali jamila mzirai
amesema mnamo 5 may mwaka hu mshitakiwa alikutwa na nyara hizokuwa na thamani
ya milioni 90 zenye uzito wa kilo 20
Mahakamna
ilimtaka mshitakiwa kutokujibu lolote juu ya shitaka linalo mkabili kwa kuwa
mahakama hiyo hauikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo la kufuatia shitaka
lenye thamani ya zaidi ya milioni 10
Wakili
ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika kesi hiyo imehairisha mpaka tarehe 23 mei mwaka
huu na mshitakiwa amerudishwa mahabusu.
Wiki
iliyopita jeshi la polisi lilipowakamata mchungaji na watuhumiwa wenzake,ilidaiwa
kuwa majina yatawekwa hadharani na polisi mara baada ya upelelezi kukamilika.
Mwandishi: Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOSPOT.COM
Comments