DIWANI NA MWENYEKITI WA KIJIJI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO WATAKIWA KUACHA TOFAUTI ZAO ZA KISIASA,WAANDISHI WA HABARI KUFUKUZWA MKUTANO WA HADHARA WANANCHI WANG'AKA
Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Nsimbo imewataka Mwenyekiti wa Kijiji cha Muungano Bw Makalai Njile na Diwani
wa Kata ya ibindi Mh, Justin Shinje Kuachana
na Chuki za Kisiasa na badala yake wafanye kazi ya kutatua kero za wananchi
wao.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa
halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh Raphael Kalinga wakati akitolea ufafanuzi Kuhusu Mgogoro uliopo wa wananchi
Kumkataa Mwenyekiti wa Kijiji hich.
Katika hatua nyingine Mh,Kalinga
amesema kitendo cha kuwazuia wandishi wa habari Kufika Katika Mkutano wa
hadhara wa Kijiji hicho uliofanyika May 21 Mwaka huu na diwani wa Kata hiyo
Kinapingana na haki ya kikatiba kupokea na Kutoa habari kwa umma kupitia vyombo
vya habari hapa nchini.
Aidha Mh,Kalinga amesema tayari Mgogoro uliopo baina ya Mwenyekiti wa
Kijiji hicho na Diwani wa Kata ya Ibindi Ulishafikishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya
Mlele tayari kwa Kufanyiwa Kazi.
Hata hivyo Mh,Kalinga amesema bado
mwenyekiti wa Kijiji cha Muungano Bw,Makalai Njile anatambulika Kisheria kama
mwenyekiti halali.
Kwa upande wa wananchi waliokuwepo
katika mkutano,wameelezwa kutoridhishwa na kitendo cha diwani wa kata hiyo
kuwazuia waandishi wa habari kushiriki kuandika habari za mkutano huo licha ya
kuwa mwenyekiti wa kijiji ambaye kisheria ndiye mwenye mamlaka ya kuitisha
mkutano kuwa na taarifa za uwepo wa mwaandishi wa habari.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments