WATU 5 WAKIWEMO WATATU WENYE KADI 19 ZA ATM ZA BENKI WANASWA NA JESHI LA POLISI KATAVI
WATU
watatu wakazi wa tarafa ya kashaulili wilaya ya Mpanda mkoani Katavi
wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa na kadi za ATM 19 za watu tofauti.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Damas Nyanda amethibitisha Kukamatwa kwa watuhumiwa
hao ambao pia wamekutwa za Kadi hizo na fedha Taslimu Kiasi cha Shilingi
milioni 3,680,000.
Katika
hatua nyingine Kamanda Nyanda amesema jeshi la polisi limewakamata watu wawili
wakazi wa Mji wa Zamani kwa Kosa la Kukutwa na Nyara za Serikali pamoja na Bang
vikiwa vimehifadhiwa kwenye kopo.
Jeshi
la Polisi Mkoani Katavi linatoa wito kwa wananchi Kutoa taarifa za uhalifu ili
Wachukuliwe sheria.
Hata hivyo watuhumiwa majina yao
hayajatajwa kwa sababu za kiuchunguzi zaidi.
Mwandishi : Issack Gerald Bathromeo
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments