WALIMU MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVIWAMEIOMBA SERIKALI KUWAPANDISHA VYEO WANAPOKUWA WAMEKIDHI VIGEZO.
WALIMU
wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuwapandisha cheo
wanapokuwa wamekidhi vigezo pamoja na kutengenezewa vitambulisho vipya vya kazi.
Wamesema
hayo jana katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Malando Manispaa ya
Mpanda kilichokuwa na lengo la
kujadili changamoto za walimu.
Aidha
wameongeza kuwa kutopandishwa cheo ni sehemu ambayo inamnyima haki mfanyakazi
wakati ni haki yake.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda Bw.Lauteri Kanoni amesema ili mfanyakazi yeyote apandishwe cheo
ni lazima aonyeshe bidii ya kufanya kazi.
Wakati
huo huo Kanoni ametumia nafasi hiyo kuwataka watumishi hewa katika manispaa ya
Mpanda kurejesha fedha zote ambazo wamelipwa na serikali kipindi wakiwa kazini.
Mwandishi : Vumilia Abel
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments