VIONGOZI SERIKALI ZA VIJIJI WILAYANI MPANDA WATAKIWA KUTOKIUKA SHERIA ZA UGAWAJI WA ARDHI
VIONGOZI
wa serikali za vijiji wilaya ya Mpanda
Mkoani Katavi wametakiwa kutokiuka utaratibu
wa kisheria katika ugawaji wa ardhi kwa wannchi.
Hayo
yameelezwa na mbunge wa jimbo la Mpanda
vijijini Mh.Moshi Suleman Kakoso wakati
akihojiwa na kituo hiki kuhusiana
na jitihada zinazochukuliwa na serikali kwa baadhi ya viongozi wa vijiji , na Kata ambao wamekuwa sehemu ya chanzo cha migogoro hiyo.
Aidha ameongeza
kusema kuwa serikali inapaswa kushughurikia migogoro hiyo halaka iwezekanavyo.
Hayo
yanakuja ikiwa migogoro mingi ya ardhi inayotokea kwa kiasi kikubwa Wilayani
Mpanda ikichangiwa na viongozi hao wakati
mwingi9ne kugawa viwanja kwa zaidi ya mtu mmoja katika eneo moja.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments