MALIASILI KATAVI WATUHUMIWA KUTEKETEZA ZAIDI YAN NYUMBA 40 NA MALI ZA RAIA ZILIZOKUWA NDANI
KAYA
zaidi ya 40 zimechomwa moto na mali
zilizokuwa ndani Katika kijiji cha Misanga Kata ya Tongwe Halmashauri ya
Tanganyika na watu wanaosadikika kuwa ni maliasiri.
Wakizungumza
baadhi ya wakazi wa eneo hilo kijiji hicho wakazi hao wamesema wamesikitishwa
na kitendo hicho kutokana na kukosa mahali pa kuishi ambapo wameiomba serikali
kuingilia kati suala hilo.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho Bw.Kwabi Mabula amesema tukio hilo limetokea akiwa hayupo
kijijini hapo ambapo amesema hii ni mara ya pili kutendewa kitendo hicho katika
kijiji chake.
Hata
hivyo mwenyekiti huyo ameitaka serikali kufika eneo la tukio ikiwa ni pamoja na
kujiridhisha na kuonesha mipaka ya kijiji hicho ili kuondoka migogoro
inayojitokeza.
Kwa
upande wake diwani wa kata hiyo Bw.Frank Markley Kibigazi amesema atafuatilia suala hilo ili kupata
ufumbuzi nakuwataka wananchi walioko nje ya bikoni kurudi katika vijiji
vinavyotambulika.
Aidha
diwani huyo ametaja maeneo ambayo serikali hairuhusu mwananchi yeyete kuishi
eneo hilo ni Kamama,Mlofyesi,Ijamba,Kansombo pamoja na Mnimba.
Naye
MBUNGE wa jimbo la Mpanda vijijini Mh .Moshi Suleman Kakoso amesema waziri wa
mali asili na utalii kwa kushirikiana
na wizara ya mali asili wanatarajia kufanya ziara ya kuangalia
migogoro iliyoko ndani ya wilaya ya Mpanda ili itatuliwe.
Ametoa
Kauli hiyo wakati akihojiwa na MPANDA
RADIO FM Kuhusu Mpango wa Serikali wa
kutatua migogoro ya aridhi kwa
wakazi wanaoshi katika maeneo ya hifadhi
ikiwa ni pamoja na baadhi ya wananchi kuchomewa nyumba zao Katika kijiji cha Misanga Kata ya Tongwe
Katika Halmashauri ya Tanganyika.
Aidha
Mh.Kakoso ametoa wito kwa wananchi wanaoshi maeneo uhifadhi wa mktaba wa DWMA
kama vile Sibwesa,kesekese,kaseganyama pamoja ya Kabage na baadhi ya maeneo
mengine yenye mkataba huo serikali inaendelea na utaratibu ili wananchi wa
maeneo hayo waishi kwa uhuru.
Mkoa
wa Katavi ni miongoni mwa mikoa yenye migogoro mingi ya aridhi , ziara hiyo ya
waziri itasaidia kuondokana na migogoro
ambayo imekuwa changamoto kubwa katika mkoa wa katavi.
Matukio
ya kuchomwa nyumba za wakazi mkoani Katavi
siyo mara ya kwanza ambapo mwaka 2013 wakazi wa kijiji cha Luhafe
walichomewa nyumba zao pamoja na mali zilizokuwemo.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments