WIZI WAENDELEA KULINDIMA MPANDA WAHUSIKA MAHAKAMA YAENDELEA KUFANYA KAZI YAKE KWA WATUHUMIWA
MAHAKAMA ya mwanzo mjini Mpanda mkoani
Katavi inamshikilia mtu mmoja kwa kosa la wizi wa mfugo wenye
thamani ya shilingi elfu arobaini na tano.
Akisoma shitaka hilo mbele ya mbele ya hakimu
mwandamizi Mh Davi Mbembela,mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi Pc Elineema
amemtaja mshitakiwa kuwa ni Ernest Daudi (41) mkazi wa Kawajense Mjini Mpanda.
Ameongeza kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo
February 23 mwaka huu maeneo ya mtaa na
kata ya Kawajense ambapo aliiba mbuzi mmoja mali ya Juma Fundisha.
Sanjari na hayo mshtakiwa amekana kosa na amerudiswa
rumande kwa kushindwa kutimiza vigezo vya dhamana ambapo mahakama imeahilisha
shtaka hilo hadi itakapotajwa tena juni 2 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments