WATUHUMIWA WAWILI KATAVI AKIWEMO MCHUNGAJI KANISA LA MORAVIAN MBARONI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO YAKIWA YAMEHIFADHIWA KANISANI.


JESHI la Polisi mkoa wa Katavi linawashikilia watu wawili akiwemo mchungaji wa kanisa la Moravian Usevya mkoani Katavi kwa kosa la kukutwa na vipande 11 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogram 20.3.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini Kwake, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Damas Nyanda amesema meno hayo yalifichwa katika ofisi ya kanisa hilo.
Aidha Kamanda Nyanda aliongeza kwa kusema kuwa watuhumiwa wote majina yao yameifadhiwa kutokana na sababu za kiusalama.
Watuhumiwa wa nyara hizo za serikali ambazo thamani yake haijajulikana mara moja,wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili.
Wakati huo huo Kamanda wa Mkoa wa Katavi alitoa kwa jamii kuacha mara moja tabia ya kujihusisha na biashara haramu za magendo pamoja na uharibifu wa rasilimali za Taifa ikiwemo vitendo vya ujangiri na badala yake jamii ijikite kwenye uwajibikaji kwa njia halali.
Mwandishi :Alinanuswe Edward
Mhaririri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika  na P5 TANZANIA MEDIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA