JIONEE HII KALI: WAKAZI MTAA WA MSASANI MANISPAA YA MPANDA WATESWA NA KUNGUNI,WAOMBA SERIKALI IWASAIDIE DAWA YA KUWAUA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,wakazi
wa Mtaa wa Msasani Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani
Katavi,wameiomba serikali kuwasaidia kupatikana dawa ya kuua wadudu aina ya KUNGUNI ambapo walisema kuwa
wameshindwa kupata hata usingizi usiku.
Wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda Radio Fm,walisema kuwa
wametumia dawa ya kila aina lakini wadudu hao wameshindikana kuuwawa na
kutokomezwa kabisa.
Baadhi ya wakazi waliozungumza na
waandishi wa habari kwa nyakati tofauti kuhusiana na hali hio ni pamoja na
Zabibu Said(56),Philbert John(36),Elisha Kenya(47),Taus Jimack(28) ambao
walisema kuwa tatizo la kunguni limeathiri hata wanafunzi kwani wanasinzia
darasani wanapokuwa wanasoma ambapo usingizi unasababishwa na kutolala usiku
kwa sababu ya wadudu hao.
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wa
serikali ya mtaa huo Bi.Fortunata Willium alithibitisha kuwepo kwa kunguni hao
katika mtaa huo hata nyumbani kwake ambapo alisema kuwa wamezungumza ili
serikali iwapatie msaada wa dawa ya kuua wadudu hao wakorofi.
Hussein Jamli Kweka mmoja wa wamiliki
wa nyumba za kulala wageni maarugu kama GUEST katika Manispaa ya Mpanda,yeye ni
mmiliki wa nyumba ya kulala wageni ya Grali Lodge(TWO IN ONE) alithibitisha
kuwepo kwa kunguni katika mtaa wa Msassani na hata katika nyumba zake za kulala
wageni ambapo alisema kuwepo kwa kunguni katika nyumba yake ya kulala wageni
kumemuathiri katika suala la kipato ambapo wateja wengi wamekuwa wakikimbia
kutokana na wadudu hao kuwa wasumbufu kwa wageni wanaolala mahali hapo.
Hata hivyo chanzo cha wadudu hao
kinasemekana ni kuwepo kwa uchafu ndani ya nyumba hususani katika vitanda vya
kulalalia licha ya kuwa halijathibitishwa na wataalamu wa afya.
Idadi kubwa ya wakazi waliozungumza
na Mtandao huu sanjari na Mpanda Radio walitaja
vyandarua vya msaada kuwa chanzo cha kunguni hao kwa kuwa vyumba ndani ya
nyumba au wakazi wasiotumia vyandarua hivyo hawana kunguni ndani ya nyumba hata
mmoja ambapo waliongeza kuwa kabla ya kugawiwa vyandaru ahivyo kunguni
hawakuwepo.
Miongoni mwa dalili na madhara ya kunguni ni pamoja na Ugonjwa wa mabaka mwili mzima,Upungufu
wa hewa,Kufura macho,Kusokotwa na tumbo
Mawasiliano kati ya Idara ya Afya na waandishi
wa habari yanaendelea ili kuliangazia suala hili ikiwa kuna uwezekanao wa
kuwasaidia wakazi hao.
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM usikose mwendelezo wa suala hili kupitia hapahapa
Comments