WIKI YA WAUGUZI MKOANI KATAVI YAZINDULIWA WAGONJWA KUPATIWA MATIBABU BILA MALIPO HADI MEI 12 KILELE CHA MAADHIMISHO
WAUGUZI na Madaktari Wilayani Mpanda
Mkoani Katavi wametiwa moyo wa kufanya kazi kwa bidii na kupuuzia maneno na
vitendo vya watu wanaowakatisha tamaa ya kufanya kazi za utoaji huduma ya afya
kwa ufanisi.
Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi
Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Estomihn Chang’a ambaye
amemwakilisha Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo aliyetakiwa kufungua maadhimisho hayo ya Wiki ya wauguzi Duniani ambapo ufunguzi huo
umefanyika katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Bw.Chang’a amesema ni wakati wa
wauguzi na madaktari kufanya kazi bila kujali matukio na hali inayolenga
kuwakwamisha katika kutoa huduma za afya kwa Wananchi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Dk.Naibu Mkongwa,akizungumza kwa niaba ya wauguzi
na madaktari Wiaya ya Mpanda,amesema kuwa malengo yao muda wote ni kuhakikisha
wanafanya kazi kwa kutoa huduma iliyo bora na kwa bidii bila kujali watu
wanawakatisha tama wanapokuwa kazini.
Awali akisoma taarifa ya Maadhimisho
hayo,Mwenyekiti wa chama cha Wauguzi Tanzania TANA Mkoani Katavi Dk.Augustina Thomas,pamoja na kusema kuwa chimbuko la
Maadhimisho yaliyoasisiwa na mwaasisi Dk.Florence Nightngely aliyezaliwa mwaka
1820,amesema kuwa lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuonesha kazi nzuri za
kiuuguzi na kusaidia jamii kujua elimu ya afya zao kwa ujumla.
Kwa upande wa idara mbalimbali ambazo
zimewasilisha taarifa kwa mgeni rasmi zimeonesha kuwa kumekuwepo na mwitikio
katika kupata vipimo na matibabu ya magonjwa yanayowasumbua.
Katika taarifa za idara hizo,idara ya
afya ya uzazi na mtoto licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa
kutoa huduma ikiwemo watu kuwa na woga wa kujitokeza kupima magonjwa ya
saratani yashingo ya kizazi,kwa mwaka 2016,wamefanikiwa kutoa huduma kwa watu
wapatao elfu 18.
Zaidi Mratibu wa Afya ya uzazi na
mtoto Wilaya ya Mpanda Dk.Gravina Kamande amebainisha.
Hata hivyo wito umetolewa kwa wakazi
Mkoani Katavi kuendelea kujitokeza kuchangia damu salama ili kunusuru wagonjwa
wenye uhitaji wa kuongezewa damu huku wenye matatizo ya meno nao wakitakiwa
kuzingatia kanuni za afya ambapo katika takwimu ambayo imetolewa na Mika John Mwanyama ambaye ni mkuu wa idara ya
kutibu meno inaonesha kuwa kuanzia mwaka 2013 katika Wilaya ya Mpanda watu 21
wamefariki dunia kutokana na tatizo la meno kati ya hao 7 wakiwa ni wanawake
ambapo kati ya hao 7 wakiwa ni wanawake wajawazito wakipoteza maisha huku walio
wengi wakipoteza maisha kutokana na kuchelewa kupata huduma katika hospitali
zilizothibitishwa wakipata huduma mitaani ambazo ni hatari.
Katika maadhimisho
hayo,vipimo,matibabu na ushauri nasaha vinatolewa bila malipo kwa kipindi chote
cha maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani kuanzia Mei 05 hadi 12 ambapo Mganga
Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Dk.Naibu Mkongwa amewahakikishia wanakatavi
Kuwa dawa zipo za kutosha kwa watakaofika hospitalini hapo kupatiwa matibabu
bila malipo.
Kilele cha Wiki ya Mauguzi
duniani kinatarajia kufikia tamati mei
12 mwaka huu ambapo Mgeni Rasmi katika MKoa wa Katavi akitarajia kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Katavi huku mgeni rasmi kitaifa akiwa ni Rais wa Tanzania Dk.John Pombe
Magufuli wakati maadhimisho hayo yatakapokuwa yakifanyikia mkoani Geita.
Mwandishi : Issack Gerald Bathromeo
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA MEDIA
Comments