BREAKING NEWS :WANNE MBARON MPANDA KWA UKIUKWAJI BEI ELEKEZI YA SUKARI
WAKATI
Serikali ikiendelea kupambana na watu wanaoficha sukari manispaa ya Mpanda
mkoani katavi imewakamata
wafanyabiashara 4 ambao wanakiuka bei
elekezi ya serikali ya kuuza sukari.
Afisa
biashara wa Manispaa ya Mpanda Bw.Mtana
Noeli amesema watu hao wamefikishwa kituo cha
polisi kwa ajili ya hatua za kisheria zaidi
Aidha amesema kuwa
kutokana najitihada zilizo fanyika za kukagua sukari ambayo imefichwa
katika manispaa ya mpanda bado hawaja
baini kiasi chochote ambacho kimefichwa.
Hata
hivyo majina ya watu hao hayajawekwa hadharani.
Mwandishi:Issack Gerald
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kufuatilia
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM upate habari hizi na nyinginezo
Comments