Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania IGP Ernset Mangu Na.Issack Gerald-Katavi MKUU wa jeshi la polisi nchini Inspekta Jenerali Ernest Mangu anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Katavi kuanzia tarehe 9 hadi 11 mwezi huu. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Katavi,ASP. Dhahiri Kidavashari, imesema kuwa katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, IGP Ernest Mangu, atakuwa na fursa ya kuzungumza na wadau mbali mbali katika hoteli ya Lyamba Lya Mfipa majira ya jioni. Katika hafla hiyo waalikwa watapata chakula cha jioni pamoja na Inspekta Jenerali wa polisi hapa nchini.