MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA TANO- 20,162 KATI YA 22,596 WAJIANDIKISHA MAKAZI MAPYA KATUMBA
Wakazi wa makazi mapya ya Katumba wakijandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura |
WANANCHI
20,162 kati ya 22,596 sawa na asilimia 89 ya wakazi wapya, Wilayani Nsimbo
Mkoani Katavi wamejiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
Takwimu
hizo zimetolewa Jumanne ya wiki hii na na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Nsimbo Bw. Hamis Mnubi wakati akizungumza na P5 TANZANIA.
Bw.
Mnubi amefafanua sababu ya kutofikia lengo la uandikishaji kuwa baadhi ya
wananchi wa makazi mapya walijiandika kwenye
kata zilizohusika katika zoezi la awali.
Zoezi
hili limezihusisha kata za Katumba, Kanoge, na baadhi ya vijiji vya kata za
Mtapenda na Litapunga.
Comments