MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA PILI-WANNE WASHIKILIWA NA POLISI KATAVI KWA KUPORA ZAIDI YA MILIONI 7,SILAHA ZA KIVITA PIA ZAKAMATWA
Na.Issack Gerald -KATAVI
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi
linawashikilia watu wanne wanaosadikika kuwa majambazi Wilayani Mpanda kwa
tuhuma za kujeruhi na kupora kiasi cha shilingi milioni saba.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Dhahiri
Kidavashari,amesema Jumatatu ya wiki hii kuwa tukio hilo limetokea katika kijiji
cha Vikonge kata ya Kabungu.
Kamanda Kidavashari aliwataja
waliokamatwa katika msako wa jeshi la polisi kuwa ni Mayunga Saguda Makobo(44)
mkazi wa Mnyagala,Halila Tiga Bujoribu(33) na Mnyaga Maziku(30) wakazi wa
Luhafe na Shija Mahoma(30) mkazi wa Kawajense.
Amesema watu hao wanaosakika kuwa
majambazi walikuwa wakitumia silaha mbili za kivita aina ya SMG UA-3379 yenye
risasi 13 na SMG namba 19111685 yenye risasi 23 ambazo zote zimekamatwa.
Wakati huohuo wakazi Mkoani Katavi wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano
kwa jeshi la Polisi kubaini uharifu.
Comments