MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA NNE,UBAKAJI WA WANAWAKE,WIZI WAKITHIRI POLISI JAMII WAKACHA ULINZI
NA. Issack Gerald-MPANDA
Kukosekana kwa uongozi imara katika
sekta ya ulinzi na usalama,kumeababisha vitendo vya wizi na ubakaji kwa
wanawake kukithiri katika mtaa wa Msasani Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.
Hayo yameelezwa jana na wakazi wa
Mtaa huo wakati wakizungumza na P5
TANZANIA Mtaani hapo.
Wamesema usalama umetoweka baada
ya na Askari wa Jeshi la polisi
jamii,kusitisha kufanya ulinzi kufuatia waharifu wanaowakamata kutochukuliwa
hatua za kisheria sambamba na kutopatiwa michango ya kujikimu wakati wa
shughuli ya ulinzi.
Naye Mwenyekiti wa mtaa huo Jonadi
Makoli amesema usalama umedhorota kutokana na wakazi wa mtaa huo kukuika
maazimio waliyojiwekea mwezi Aprili mwaka huu katika mkutano wa hadhara wa
kuwachangia vijana wa polisi jamii.
Comments