MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA SITA-JAMII YATAKIWA KUWATAMBUA WATOTO WENYE ULEMAVU
Na.Issack Gerald-MPANDA.
JAMII
Mkoani Katavi imeombwa kutambua uwepo wa watoto wenye ulemavu, ili kuwapatia
haki za msingi sawa na watoto wengine.
Ombi
hilo limetolewa na Mratibu Elimu jumuishi Mkoa wa Rukwa na katavi Raphael
Fortunatus wakati akizungumza na P5
TANZANIA Alhamisi ya wiki hii katika ofisi za Shirika la IFI lililopo Manispaa ya Mpanda
Mkoani hapa.
Amesema
shirika la hilo linafanya kazi ya
kubaini na kutambua uwepo wa watoto hao, kuwaandikisha shule na kutoa elimu kwa
watoto hao na jamii kwa ujumla juu ya haki za watoto wenye walemavu.
Aidha
bw. Fortunatus amesema kupiatia mikutano ya hadhara, pamoja na Mabaraza ya
watoto wenye ulemavu, Shirika la IFI limewafikia watoto 112 na kuwapatia
misaada mbalimbali.
Comments