MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA KWANZA-MWANAMKE AKATWA PUA,ACHANWA SIKIO MMEWE AKATAA KUELEZA SABABU
Na.Issack Gerald-MPANDA.
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina
la Magdarena Joseph Mkazi wa Mwamkulu Senatalumbanga Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi
amekatwa pua na kuchanwa sikio na mme wake Lukona Machimba,Kutokana na ugomvi
wa kifamilia.
Akizungumza na P5 TANZANIA Jumatano ya wiki hii,Bi. Magdalena amesema chanzo cha
ugomvi ni ukosefu wa usafiri mara baada
ya kulala Mjini Mpanda.
P5 TANZANIA imezungumza na Bw. Lukona
ambaye ni mme wa Mwanamke huyo, kwa njia
ya simu juu ya tukio hilo ambapo hakuonesha ushirikiano na kudai ana shughuli.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa
kijiji hicho Bw. Harun Festo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amietaka
jamii kuacha vitendo vya kujichukilia sheria mkononi, pamoja na vitendo vya
ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Comments