MATUKIO 6 MAKUU YALIYOTOKEA KATAVI WIKI HILI LA TATU KATIKA SISA MGOMBEA UBUNGE CUF MPANDA ASHINDWA KUREJESHA FOMU,AFISA UCHAGUZI ALONGA
NA. Meshack Ngumba-MPANDA
Chama cha Wananchi Cuf Kimeshindwa
Kurejesha fomu ya Mgombea wa Ubunge Kupitia chama hicho Katika Jimbo la Mpanda
Mjini Katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi manispaa ya Mpanda.
Akizungumza kwa Njia ya Simu na Kituo
hiki Afisa Uchaguzi Katika Manispaa ya Mpanda bwana Clavery Reginald amesema
hadi Kufikia Muda wa Kufunga zoezi la Urejeshwaji wa fomu za wagombea ni Vyama
vinne tu Vilivyorejesha fomu za Wagombea
wao ndani ya Muda uliopangwa.
Kwa Mjibu wa ratiba ya tume ya taifa
ya Uchaguzi Kesho Augost 22 Mwaka huu Vyama vyote vya siasa vinaruhusiwa Kuanza
kampeni za Kuwanadi wagombea wao Kuanzia Ngazi ya Madiwani,wabunge na Rais.
Comments