YASIKUPITE,MATUKIO WIKI HII KATAVI KATIKA SIASA,UCHUMI,MAKUNDI MAALUMU
SUALA LA SIASA
Na.Issack Gerald-Katavi
WAGOMBEA
wa nafasi mbalimbali za uongozi Mkoani Katavi
wameaswa kuacha kutoa rushwa ili kujipatia ushindi katika uchaguzi ujao.
Hayo
yamesemwa na baadhi ya viongozi wa dini mkoani hapa Jumatano wakati wakizungumza na
P5 TANZANIA.
Miongoni
mwa viongozi hao wa dini ni Askofu mkuu wa makanisa ya New haverst nchini
askofu Laban Ndimubenye, amesema wagombea wanaotumia rushwa kuingia madarakani
hawafai katika maadili ya nchi.
Naye
Kaimu sheikh mkoani katavi wananchi
waliojiandikisha wanapaswa kuwa tayari kwenda kumchagua kiongozi wanayemtaka
ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KATIKA SEKTA YA USALAMA BARABARANI
KIKOSI
cha usalama barabarani mkoani Katavi kimewatadharisha madereva kuacha kutumia vilevi
ambavyo ndiyo chanzo cha ajali.
Akizungumza
na P5 TANZANIA katika mahojiano,mmoja wa wawakilishi kutoka kikosi cha
usalama barabarani Pc Dotto Anderson amesema ulevi unaweza kuepukika bila
shuruti.
PC
Anderson ameongeza kusema kuwa ajali nyingi zimekuwa zikisababishwa na ulevi,
mwendo kasi na uelewa mdogo wa sheria za usalama barabarani.
Aidha
abiria katika vyombo vya usafiri na jamii kwa ujumla wameaswa kutoa taarifa
pindi ukiukwaji wa sheria za barabarani unapofanywa.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
WAKULIMA ZAO LA TUMBAKU MPANDA WAENDELEA KUGUBIKWA NA UMASKINI
Na.Issack Gerald
WAKULIMA wa zao la tumbaku mkoani Katavi wameendelea
kubakia katika umasikini licha ya
vyama vya ushirika na serikali kudai kuwepo kwa mafanikio katika sekta ya
kilimo.
Wakizungumza na P5 TANZANIA Alhamisi
ya Wiki hii baadhi ya wakulima wamekosoa mwenendo wa masoko ya zao hilo kwa kusema
kuwa hauwanufaishi kama wakulima licha ya kuzinduliwa kwa Masoko ya zao hilo
hivi Karibuni.
Kutokana na Malalamiko hayo Mmoja wa
wajumbe wa chama cha msingi Mpanda kati cha Majalila bwana Emmanuel Kanyuka
amesema hali iliyopo sasa katika Masoko ya tumbaku ni tofauti na ilivyokuwa
hapo awali licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima
hao.
Mamlaka ya Vyama vya Ushirika Mkoani
hapa zimekuwa zikilalamikiwa na wakulima kwa kuweka mbele maslahi yao badala ya
Mkulima.
Source,Alinanuswe Edward,Editor Mark Ngumba.13/8/2015.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
JAMII WILAYANI MLELE YASHAULIWA KUWASAIDIA WASIOJIWEZA.
Na.Issack Gerald
Jamii Mkoani Katavi imeshauriwa
Kusaidiana na taasisi zisizo za Kiserikali kusaidia watoto yatima na wanaoishi
katika mazingira magumu kwa kutoa Misaada ya Kijamii ili Kupunguza idadi ya
Watoto wa mitaani.
Akizungumza na P5 TANZANIA Alhamisi ya wiki hii,Mkurugenzi wa shirika la usevya Development Society
UDESO lenye makao makuu yake Wilayani Mlele Mkoani Katavi bwana Edeni Ezekiel
Waimba.
amesema Jamii inatakiwa kuacha kuwa
tegemezi kwa Serikali na Mashirika
binafsi kwa Kujiunga na Vikundi mbalimbali vya Kusaidia watu wa Makundi
maalum wakiwemo watoto yatima.
Bw. Waimba amesema kuwa kwa mwaka 2014/2015 Shirika la UDESO limetoa
misaada mbalimbali kwa watoto takribani 1500.
Comments