IGP MANGU AHIMIZA AMANI KATAVI
NA.Issack Gerald-Katavi
MKUU
wa jeshi la polisi nchini Inspekta jenerali Ernest Mangu, amesema kila mtu atimize
wajibu wake ili kuhakikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka
huu, unafanyika kwa amani na utulivu.
IGP
Mangu ametoa kauli hiyo juzi katika hoteli ya Lyamba Lya Mfipa mjini Mpanda,
wakati akizungumza na wadau mbali mbali wa jeshi la polisi wakati wa chakula
cha usiku kilichoandaliwa na jeshi la polisi.
Awali
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dk. Ibrahim Msengi alimueleza Mkuu wa jeshi la polisi
nchini kuwa hali ya usalama mkoani Katavi ni shwari kutokana na kazi nzuri
inayofanywa na kamati ya usalama ya mkoa, na kuwataka wakazi wa mkoa wa katavi
kuendeleza amani iliyopo.
Hafla
hiyo imehudhuriwa na wadau mbali mbali, wakimwemo viongozi wa dini, mashirika
yasiyo ya kiserikali, taasisi za fedha, wafanyabiashara, pamoja na waandishi wa
habari.
Comments