UVAMIZI OFISI ZA CCM SUMBAWANGA RUKWA,SAMANI ZA MWENYEKITI VYATUPWA NJE
Na.Mwandisi wetu-SUMBAWANGA.
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya
Sumbawanga mkoani Rukwa wanaosadikiwa kuwa ni wanachama wa chama cha Mapinduzi,
juzi wameivamia ofisi ya chama hicho ya wilaya ya Sumbawanga mjini.
Wananchi hao walitoa samani zote
zilizoko kwenye ofisi ya mwenyekiti wa wilaya hiyo na kuzitupa nje, kwa
kumtuhumu kuwa ameongoza vikao vilivyokata jina la mbunge anayemaliza muhula
wake Aeshi Hilal aliyeshinda kwenye kura za maoni.
Wakiongea kwa jaziba mbele ya ofisi
hizo za CCM, Wilaya ya Sumbawanga katika
barabara ya sokoine mjini Sumbawanga, wamesema hata siku moja hawawezi
kuvumilia vitendo vinavyofanywa na Mwenyekiti wa CCM, wa wilaya hiyo Bw, Selemani
Kilindu kwa chuki binafsi.
Comments