IGP MANGU ZIARANI KATAVI KESHO NA KESHO KUTWA
Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania IGP Ernset Mangu |
Na.Issack Gerald-Katavi
MKUU wa jeshi la polisi nchini
Inspekta Jenerali Ernest Mangu anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili
mkoani Katavi kuanzia tarehe 9 hadi 11 mwezi huu.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya
habari na kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Katavi,ASP. Dhahiri Kidavashari,
imesema kuwa katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, IGP Ernest Mangu, atakuwa na fursa ya kuzungumza na wadau mbali
mbali katika hoteli ya Lyamba Lya Mfipa majira ya jioni.
Katika hafla hiyo waalikwa watapata
chakula cha jioni pamoja na Inspekta Jenerali wa polisi hapa nchini.
Comments