MAJAMBAZI YAPORA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI SABA,YAJERUHI PIA
Na.Issack Gerald-KATAVI
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi
linawashikilia watu wanne Wilayani Mpanda kwa tuhuma za kujeruhi na kupora kiasi
cha shilingi milioni saba.
Akithibitisha kutokea kwa tukio
hilo,Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Dhahiri Kidavashari,amesema kuwa tukio
hilo limetokea jana katika kijiji cha Vikonge kata ya Kabungu.
Kidavashari amewataja waliokamatwa
katika msako wa jeshi la polisi kuwa ni Mayunga Saguda Makobo(44) mkazi wa
Mnyagala,Halila Tiga Bujoribu(33) na Mnyaga Maziku(30) wakazi wa Luhafe na
Shija Mahoma(30) mkazi wa Kawajense.
Amesema kuwa watu hao wanaosakika
kuwa majambazi waliokuwa wakitumia silaha mbili za kivita aina ya SMG UA-3379
yenye risasi 13 na SMG namba 19111685 yenye risasi 23 walifanya uporaji huo kwa wafanyabiashara
Siasa Simon Kasumuni(24) ameporwa shilingi Milioni Tano,simu moja aina ya
Techno na Kadi ya benki ya CRDB wakati huo Edward Mnonga(37) ameporwa zaidi ya zshilingi
Milioni mbili,simu moja aina ya Techno,kitambulisho cha kupigiakura ambapo kwa
upande wake pia alijeruhiwa kwa kupigwa fimbo mkononi na kumsababishia maumivu
makali ambapo wote walikuwa wamelala nyumbani kwa Mnyaga Maziku Mkazi wa Luhafe.
Wakati huohuo Kamanda Kidavashari
ametoa wito kwa wakazi Mkoani Katavi waliopo
mbali na vituo vya jeshi la polisi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la
polisi kubaini uharifu kabla ya haujatokea ili kuudhibiti.
Comments