SERIKALI,JAMII WAOMBWA KUWASAIDIA WATOTO YATIMA
NA.Issack Gerald-NSIMBO
Serikali na Jamii kwa ujumla Mkoani
Katavi imeombwa kutoa misaada kwa watoto
yatima na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Ombi hilo limetolewa na Mratibu wa Kituo cha kulelea watoto yatima na
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi GUESTMAN kilichopo kata ya Litapunga Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,
Buruda Moses wakati akizungumza na mpanda redio kwa njia ya simu.
Moses amesema watoto hawa wanatakiwa
kupatiwa mahitaji sawa kama watoto wengine sambamba na kuoneshwa ukaribu na
upendo.
Comments