WAKULIMA,WAFUGAJI MPANDA WATOA MAONI KUHUSU SHEREHE ZA NANENANE
NA.Issack Gerald-Mpanda
SIKU
mbili baada ya maonesho ya kilimo na ufugaji
maarufu kama nane nane, baadhi ya wakulima pamoja na wafugaji Mkoani Katavi wametoa
maoni na mapendekezo kuhusu sekta ya kilimo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mapema jana wakulima hao walisema kuna umuhimu mkubwa kwa
serikali kuanza kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.
Changamoto
mbali mbali zimetajwa kuwa kikwazo kwa wakulima nchini katika kufikia adhma ya
kuzalisha mazao kwa kiwango bora.
Wametaja
changamoto hizo kuwa ni pamoja na Uhaba wa masoko, kukosekana kwa pembejeo za
kilimo pamoja na migogoro ya ardhi.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
Jakaya Kikwete akiwa mgeni rasmi katika kufunga maonesho ya nane nane kitaifa yaliyofanyika
mkoani Lindi amesema serikali itaelekeza nguvu zaidi katika kukabiliana na
changamoto za kilimo.
Comments