WANASIASA KIKWAZO UTEKELEZAJI AGIZO LA MKURUGENZI
NA. Alinanuswe Edward-Katavi
Wanasiasa wamedaiwa kuchangia kukwamisha utekelezaji wa agizo la Manispaa ya mpanda lilitolewa
mwishoni mwa mwezi mei likiwataka watu wote wanwanaosafisha magari yao katika
mto misunkumilo kuacha mara moja.
Akihojiwa na P5 TANZANIA Afisa mtendaji wa mtaa wa misunkumilo Bw Antpasi
Kalumbe amesema utekelezaji wa agizo
hilo umeingia dosari kutokana na vizingiti vya baadhi ya wanasiasa
Kalumbe ameongeza kusema kuwa mpaka
sasa hatua kali zimekwishachukuliwa kwa baadhi ya wanaokaidi licha ya kuwa na taarifa za agizo hilo.
Kwa upande wa vijana wanao jihusisha
na kusafisha magari katika mto huo wamekiri kupata taarifa hizo ambapo wamesema
kuwa wanashindwa kuondoka katika eneo hilo kutokana na hofu ya kupoteza ajira.
Comments