UHAKIKI DAFTARI LA MPIGA KURA NSIMBO WAFANYIKA
NA.Agness Mnub-KATAVI
ZOEZI la Kuhakiki taarifa katika
daftari la Kudumu la Mpiga Kura limeanza Katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
Mkoani Katavi Kufuatia Tangazo lililotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya
Zoezi hilo.
Akizungumza na P5 TANZANIA Uchaguzi Katika halmashauri hiyo Bwana Hamis Mnubi
amesema Zoezi hilo litawahusu waliokwisha Jiandikisha Kwenye Daftari la Mpiga
Kura Kwa Kutumia Mfumo mpya wa BVR.
Zoezi la Uhakiki wa Taarifa litawahusu wapiga kura waliojiandikisha
Katika daftari la Mpiga Kura lililioanza Mei 18 na Kukamilika June 17 Mkoani
Katavi,ambapo Zoezi la Uhakiki wa Taarifa lililoanza Augost 7 linatarajiwa
kukamilika Augost 11 mwaka huu.
Comments